Page 1 of 1

WATANO WANAOWANIA TUZO YA BBC YA MWANASOKA BORA AFRIKA

Posted: Sun Nov 12, 2017 5:16 pm
by ZakkyF
1. Image

Mohamed Salah: Amekuwa katika kiwango bora kwenye klabu ya Liverpool, akiwa amefunga magoli saba, na kuiwezesha Misri kufuzu Kombe la Dunia 2018, Urusi.

2. Image

Sadio Mane: Amekuwa mchezaji muhimu kwa Liverpool, na imedhihirika kuwa bila yeye klabu haifanyi vizuri baada ya kupata majeraha. Lakini pia amekuwa mhimili mkuu kwa Senegal kufuzu Komba la Dunia.

3. Image

Pierre Emerick-Aubameyang: Aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa nne kufunga zaidi ya magoli 30 kwenye ligi ya Ujerumani Bundesliga baada ya kufunga mabao 35 msimu uliopita na kutwaa kiatu cha dhahabu. Ameshindwa kuipeleka Gabon Kombe la Dunia lakini ameingia kwenye orodha ya tano bora za BBC.

4. Image

Victor Moses: Amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Antonio Conte pale Chelsea kabla ya janga la majeraha kumkumba, Nigeria imefuzu Kombe la Dunia kama Misri na Senegal na umahiri wake umemuingiza kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa BBC Afrika

5. Image

Naby Keita: Amewaacha wadau wengi wa soka midomo wazi baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu akiichezea RB Leipzig inayoshiriki Ligi ya Ujerumani Bundesliga. Liverpool ni klabu inayomtolea udenda katika harakati za kutaka kuimarisha kikosi chao.