Page 1 of 1

RONALDO BORA ZAIDI YA MAHIRI MESSI, ASEMA ALONSO

Posted: Sun Nov 12, 2017 5:01 pm
by Spotter
Image
Cristiano Ronaldo ni bora zaidi ya mchezaji mahiri Lionel Messi, kwa mujibu wa dereva wa Formula One Fernando Alonso.
Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na maestro wa Barcelona Messi wamekuwa wakilinganishwa mara nyingi, katika nyakati hizi za kisasa wawili hao wakiwa wametwaa Ballon d'Or mara tisa kwa pamoja.
Alonso bingwa wa dunia wa F1 mara mbili na mjumbe wa heshima wa Madrid, amesema hakuna shaka akilini mwake kwamba ni nani bora baina ya wawili hao.
"Cristiano ni bora zaidi ya Messi, naam," Muhispania huyo aliiambia Globo Esporte.
"Messi ana kipaji cha ajabu pia, lakini kama shabiki wa Real Madrid, wachezaji wa Real Madrid pekee ndio wanaonivutia."
Soma zaidi http://www.goal.com/sw/habari/ronaldo-b ... r1yxc77uui